15 Oktoba 2016 - 19:05
Mazungumzo kuhusu  amani ya Syria yaanza Uswisi

Urusi imesisitiza kuwa imechoshwa na siasa za kindumila kuwili za Marekani za kujinadi kupambana na Magaidi ili hali inawaunga mkono na kuwapa silaha.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Imekuwa ni kawaida kwa Marekani na washirika wake wanaounga mkono upande wa magaidi nchini Syria kuitisha usitishwaji mapambano pale tu wanapoona magaidi wanaelemewa na Majeshi ya Serikali, ambayo yanaungwa mkono na Iran na Urusi.

Mazungumzo mapya ya kutafuta njia za kumaliza mgogoro wa Syria yameanza nchini Uswisi yakihusisha Marekani, Urusi na wanadiplomasia wengine. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov walikutana mjini Lausanne na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kabla ya kukutana na wajumbe wengine kutoka  nchi zinazounga mkono upande wa magaidi zikiwemo Saudi Arabia, Uturuki, Misri, Jordan na Qatar pia katika Mkutano huo imeshikishwa Iran ambayo ni mshirika mkuu wa serikali halali ya Syria. Awali , Urusi na Marekani zilifikia makubaliano ya pamoja ya kusitisha mapigano nchini Syria lakini hata hivyo makubaliano hayo yalivunjika baada majeshi ya Marekani kufanya mashambulizi katika ngome za jeshi la Syria na kuwasaidia magaidi. Marekani ambayo ndio mchocheaji mkuu wa vita nchini Syria imesema mazungumzo hayo yameandaliwa ili kuzileta pamoja nchi zinazoathirika na mgogoro wa Syria ili kutafuta njia za kuumaliza mgogoro huo.

Urusi imesisitiza kuwa imechoshwa na siasa za kindumila kuwili za Marekani za kujinadi kupambana na Magaidi ili hali inawaunga mkono na kuwapa silaha.

Mwisho wa habari/ 291